1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KABUL: Wapiganaji wa Taliban wauawa kusini mwa Afghanistan

15 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CC1q

Hadi wapiganaji 60 wa Kitaliban wameuawa katika mashambulio ya angani yaliyofanywa na vikosi vya NATO kusini mwa Afghanistan.Polisi katika wilaya ya Kandahar wakitoa taarifa hiyo wamesema, mashambulio hayo yalifanywa wakati wa usiku katika eneo la Zherai,baada ya vikosi vya Afghanistan na NATO kuarifiwa kuwa waasi wa Taliban walikusanyika katika maeneo mawili ya wilaya hiyo.Msemaji wa NATO lakini amesema kwa wakati huu operesheni hiyo haiwezi kuthibitishwa.