1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KABUL : Wanne wauwawa katika mripuko

17 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CC9H

Takriban watu wanne wameuwawa wakati gari la Umoja wa mataifa lilipokanyaga bomu lililotegwa barabarani kusini mwa Afghanistan.

Polisi imesema wageni wawili ni miongoni mwa wahanga ambao walikuwa wakisafiri katika mji wa Kandahar wakiwa kwenye gari lenye utambulisho wa Umoja wa Mataifa wakati mripuko huo ulipotokea.

Msemaji wa Umoja wa Mataifa amesema wamekuwa wakijaribu kuyakinisha repoti hizo.