1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KABUL: Wanamgambo wa Taliban wauawa nchini Afghanistan

13 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCtG

Maafisa nchini Afghanistan wamesema zaidi ya waasi 60 wanaohusika na Taliban wameuawa katika mashambulio yaliofanywa na vikosi vya NATO na vya Afghanistan.Operesheni hiyo ya siku sita ilikuwa katika wilaya ya Paktika karibu na mpaka wa Pakistan.Maafisa katika vikosi vya kimataifa vinavyosaidia kulinda usalama-ISAF-vikiongozwa na NATO,wamethibitisha kuwa vikosi vyao vilishiriki katika operesheni hiyo lakini walikataa kutaja idadi ya hasara iliyopatikana upande wao.