KABUL: Wanamgambo 60 wa Taliban wauawa Afghanistan | Habari za Ulimwengu | DW | 23.06.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

KABUL: Wanamgambo 60 wa Taliban wauawa Afghanistan

Hadi wanamgambo 60 wa Taliban wameuawa katika mashambulizi yaliyofanywa na vikosi vya anga na nchi kavu vya NATO,kusini-mashariki mwa Afghanistan karibu na mpaka wa Pakistan.Hapo awali,vikosi vya NATO viliua wapiganaji wa Taliban 30 na uchunguzi unafanywa kuhusika na ripoti kuwa katika mashambulizi hayo,raia 25 pia waliuawa.Taarifa iliyotolewa na vikosi vya kimataifa vinavyoongozwa na NATO nchini Afghanistan imesema,inaaminiwa kuwa wanamgambo walichochea mashambulizi hayo kulenga nyumba mbili,katika wilaya ya Helmand kusini mwa nchi. Wapiganaji wa Taliban wanalaumiwa kutumia raia kama ngáo ya binadamu.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com