KABUL: Wanamgambo 50 wa Taliban wameuawa | Habari za Ulimwengu | DW | 27.07.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

KABUL: Wanamgambo 50 wa Taliban wameuawa

Zaidi ya waasi 50 walioshukiwa kuwa Wataliban, wameuawa na vikosi vinavyoongozwa na Marekani nchini Afghanistan.Kwa mujibu wa msemaji wa majeshi hayo,hakuna raia au wanajeshi waliouawa katika mapigano yaliyodumu saa 12 katika jimbo la kusini la Helmand.

Kwa upande mwingine,wateka nyara wa Wakorea wa Kusini 22 nchini Afghanistan,wamerefusha hadi Ijumaa mchana,muda wa kutimiziwa madai yao.Kwa mujibu wa msemaji wa waasi hao,serikali ya Kabul katika muda uliotolewa,iwaachilie huru Wataliban waliozuiliwa jela au sivyo,mateka watauawa.Siku ya Jumatano,watekanyara hao walimuua padri mmoja,ikisemekana alikuwa kiongozi wa kundi hilo la Wakorea ya Kusini.Wakorea hao walitekwa nyara juma moja lililopita.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com