1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KABUL: Wanajeshi wa Kijerumani wameuawa Afghanistan

19 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CC0Y

Wanajeshi 3 wa Kijerumani na raia 4 wameuawa baada ya mwanamgambo aliejitolea muhanga, kujiripua katika soko lililojaa watu,katika mji wa Kundus,kaskazini mwa Afghanistan.Wanamgambo wa Taliban wamedai kuhusika na shambulio hilo,ambalo ni baya kabisa kupata kufanywa dhidi ya majeshi ya Kijerumani tangu mwaka 2003.Kwa mujibu wa polisi,watu wengine 14 walijeruhiwa katika shambulio hilo,ikiwa ni pamoja na wanajeshi 2 wa Kijerumani na mkalimani wao.Waziri wa ulinzi wa Ujerumani,Franz Josef Jung na Kansela Angela Merkel wakiwa na huzuni mkubwa wamelaani shambulio hilo.Wakati huo huo,chama cha upinzani cha Ujerumani cha Linkspartei,kikisikitika kuhusu vifo vya wanajeshi hao,kwa mara nyingine tena kimetoa wito wa kusitisha ujumbe wa majeshi ya Ujerumani nchini Afghanistan.Kiasi ya wanajeshi 3,000 wa Ujerumani wapo kaskazini mwa Afghanistan kama sehemu ya vikosi vya amani vya NATO,nchini humo.