KABUL: Walinzi wa msafara wauawa Afghanistan
25 Agosti 2007Matangazo
Bomu lililotegwa kando ya barabara limeua Waafghanistani 2 waliokuwa wakilinda msafara wa magari ya NATO katika wilaya ya Kandahar,kusini mwa Afghanistan.Walinzi wengine 3 walijeruhiwa pia katika shambulizi hilo. Wanamgambo waliripua bomu hilo kutoka mbali.
Wakati huo huo katika wilaya ya jirani ya Helmand,wanajeshi waliwapiga risasi na kuwaua watu 2 walioshukiwa kuwa wanamgambo wa Taliban na walitaka kutega bomu kando ya barabara.