1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KABUL: Steinmeier atembelea vikosi Afghanistan

22 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CBzd

Waziri wa nje wa Ujerumani,Frank-Walter Steinmeier amekutana na Rais Hamid Karzai wa Afghanistan.Hapo awali Steinmeier,alitembelea kituo cha majeshi ya Kijerumani mjini Kundus, kaskazini mwa Afghanistan.Jumamosi iliyopita, wanajeshi 3 wa Kijerumani na raia 5 wa Afghanistan waliuawa katika shambulio la kujitolea muhanga lililofanywa mjini Kundus. Alipotembelea wanajeshi wa Kijerumani,waziri Steinmeier alisifu kazi zinazotekelezwa na vikosi hivyo nchini Afghanistan.Akasema,wanajeshi hao wamefanya maendeleo makubwa kusaidia kuijenga upya Afghanistan,tangu vikosi hivyo kupelekwa nchi hiyo kwa mara ya kwanza miaka mitano iliyopita.Wakati huo huo akaeleza waziwazi kuwa hakuna kinga dhidi ya mashambulio ya kigaidi.