1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KABUL: Spika wa bunge la Marekani ashauriana na rais wa Afghanistan.

28 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCX2

Spika wa bunge la Marekani, Bibi Nancy Pelosi yumo nchini Afghanistan ambako ameshauriana na Rais wa nchi hiyo, Hamid Karzai.

Bibi Nancy Pelosi pamoja na ujumbe wake wa bunge waliwatembelea wanajeshi wa Marekani kwenye kituo cha Bagram ambacho ndicho kituo kikubwa zaidi cha kijeshi cha Marekani nchini Afghanistan.

Kabla ya kuelekea Afghanistan, Bibi Nancy Pelosi na ujumbe wake jana walishauriana na Rais wa Pakistan, Pervez Musharraf, kuhusu hali nchini Afghanistan na pia ushirikiano wa kukabiliana na ugaidi.