1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KABUL: Shambulio la bomu limeua watu 35 nchini Afghanistan

17 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBqx

Si chini ya watu 35 wameuawa baada ya bomu kuripuka ndani ya basi la polisi asubuhi ya leo, katika mji mkuu wa Afghanistan,Kabul.Shambulizi hilo pia limejeruhi watu dazeni kadhaa.Maafisa wamesema,basi hilo lilikuwa likiwapeleka walimu kwenye taasisi ya polisi.Siku ya Jumamosi,raia wanne waliuawa katika shambulio la kujitolea muhanga lililofanywa na Wataliban dhidi ya msafara wa magari ya majeshi ya NATO mjini Kabul.Raia mwengine aliuawa baada ya wanajeshi wa Kimarekani kulifyatulia risasi,kundi la watu waliokuwa wamesimama pembeni.