KABUL: Shambulio la bomu limeua wanajeshi wa Kijerumani
19 Mei 2007Matangazo
Wanajeshi 3 wa Kijerumani na raia 4 wameuawa nchini Afghanistan.Kwa mujibu wa maafisa wa Afghanistan,mwanamgambo aliejitolea muhanga, alishambulia wanajeshi waliokuwa wakipiga doria katika wilaya ya kaskazini ya Kundus.Hadi watu 14 wengine pia walijeruhiwa katika shambulio hilo, wawili wakiwa ni wanajeshi wa Kijerumani.Kiasi ya wanajeshi 3,000 wa Ujerumani wapo kaskazini mwa Afghanistan,kama sehemu ya vikosi vya amani vya NATO nchini humo.