KABUL: Raia 16 wameuawa mashariki mwa Afghanistan | Habari za Ulimwengu | DW | 04.03.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

KABUL: Raia 16 wameuawa mashariki mwa Afghanistan

Maafisa wa kijeshi wa Marekani nchini Afghanistan wamesema,raia 16 wa Kiafghanistan wameuawa na zaidi ya 20 wamejeruhiwa kufuatia kile walichoeleza kuwa ni shambulio la utata la Wataliban.Katika taarifa iliyotolewa,maafisa hao wamesema,vikosi vya Kimarekani vilifyatua risasi katika juhudi ya kujilinda,baada ya mlolongo wa magari yao kushambuliwa na mtu aliejitolea muhanga na kufyatuliwa risasi na wanamgambo huko Jalalabad,mji ulio mashariki ya nchi.Taarifa hiyo haikueleza wazi wazi vipi raia hao wamekuwa wahanga.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com