KABUL : Polisi yawatafuta Wajerumani waliotekwa
20 Julai 2007Matangazo
Vikosi vya serikali ya Afghanistan vinawatafuta raia wawili wa Ujerumani na wenzao wa Kiafghanistan ambao wametekwa nyara katikati ya Afghanistan.
Polisi imesema watu wenye silaha waliwateka watu hao wanne katika jimbo la kati la Wardak ambapo walikuwa wakifanya kazi kwenye mradi mmoja wa maendeleo kwa ajili ya kampuni yenye makao yake mjini Kabul.
Msemaji wa wizara ya mambo ya ndani ya Ujerumani Martin Jäger amesema tume ya dharura inashughulikia kuachiliwa kwao na kwamba imeweza kukusanya taarifa mbali mbali.