1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kabul. Mullah Dadullah auwawa.

14 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CC2E

Jeshi la kimataifa la NATO nchini Afghanistan , limethibitisha kuwa kamanda mkuu wa jeshi la wapiganaji wa Taliban Mullah Dadullah ameuwawa.

Dadullah , ambaye alikuwa mjumbe katika kundi la watu kumi viongozi wa Taliban , aliuwawa katika operesheni ya kijeshi katika jimbo la Helmand.

Nato imesema kuwa kifo chake ni pigo kubwa kwa wapiganaji wa Taliban nchini Afghanistan.

Dadullah anasemekana kuwa ni mpiganaji katili ambaye alipambana na majeshi ya Urusi ya zamani katika miaka ya 1980 na alihusika na mauaji kadha kabla na baada ya kuanguka kwa utawala wa Taliban mwaka 2001.