1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KABUL: Msafara wa viongozi washambuliwa Afghanistan

18 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CC16

Mwanamgambo aliejitolea muhanga ameshambulia msafara wa viongozi wa serikali,kusini mwa Afghanistan.Mripuko wa shambulizi hilo,umeua watu watatu waliokuwa wakipita njia.Waziri wa habari wa Afghanistan Abdul Karim Khurram na Gavana wa Wilaya ya Kandahar,Assadullah Khalid walijeruhiwa kidogo tu katika shambulio hilo.