KABUL: Msafara wa kibalozi washambuliwa Afghanistan
18 Julai 2007Matangazo
Nchini Afghanistan,mshambulizi wa kujitolea muhanga maisha,ameshambulia msafara wa kibalozi wa Uturuki katika mji mkuu Kabul.Duru za polisi zikiripoti habari hiyo,ziliongezea kuwa raia mmoja wa Afghanistan alijeruhiwa katika shambulizo hilo.Baadae katika kufyatuliana risasi,mlinzi mmoja wa Kituruiki pia alijeruhiwa. Wanamgambo wa Kitaliban wamedai kuwa ndio waliohusika na shambulizi hilo ukingoni mwa mji mkuu Kabul.