KABUL: Mripuko umeua watu 6 Afghanistan
14 Machi 2007Matangazo
Mripuko mkubwa uliyotokea katika mji mkuu wa Afghanistan,Kabul,umeua watu 6 na si chini ya 9 wengine wamejeruhiwa.Mripuko huo uliyotokea karibu na kasri la rais na ofisi zingine za serikali,umeteketeza pia nyumba na maduka darzeni kadhaa.Kwa mujibu wa polisi,mripuko huo ulisababishwa na baruti katika duka linalouza silaha.Lakini afisa mmoja wa upelelezi amesema,bomu ndio lililosababisha mripuko huo.