KABUL : Mfanyakazi wa misaada wa Ujerumani auwawa | Habari za Ulimwengu | DW | 09.03.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

KABUL : Mfanyakazi wa misaada wa Ujerumani auwawa

Mfanyakazi wa misaada wa Ujerumani amepigwa risasi na kuuwawa nchini Afghanistan.

Maafisa wa serikali wamesema watu wenye silaha wememuuwa Mjerumani huyo ambaye alikuwa akifanya kazi na kundi la misaada la German Agro Action karibu na kijiji cha Mirza Wolang kaskazini mwa jimbo la Sari Pul.Washambuliaji hao pia waliwapora wafanyakazi wenzake watatu wa Kiafghanistan wakati wakiwa safarini katika magari mawili katika wilaya ya Sayyad ambapo walisimamishwa na watu hao wenye silaha.

Msemaji wa kundi hilo la msaada la Ujerumani lenye makao yake mjini Bonn amethibitisha kutokea kwa mauaji hayo.

Wakati huo huo kaskazini mwa Afghanistan mshambuliaji wa kujitolea muhanga maisha amejiripuwa karibu na msafara wa wanajeshi wa Umoja wa Kujihami wa Mataifa ya Magharibi NATO karibu na mji wa Kandahar na kujeruhi raia watano wakiwemo watoto watatu.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com