1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KABUL: Mazungumzo ya kuwaokoa mateka wa Korea Kusini yakwama

30 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBdk

Mazungumzo ya kuwaokoa mateka 22 wa Korea Kusini wanaozuiliwa na kundi la Taliban nchini Afghanstan yamekwama leo huku muda uliowekwa na wanamgambo wa Taliban kabla kuanza kuwaua ukikaribia kumalizika.

Mazungumzo ya kuwaokoa Wakorea Kusini waliotekwa nyara kusini mwa Afghanistan siku 13 zilizopita yamekwama kwa sababu ya sharti la kundi la Taliban kutaka baadhi ya wanamgambo wake wanaozuiliwa gerezani waachiliwe huru.

Kundi hilo lilikataa sharti la serikali ya mjini Kabul ikitaka liwaachie mateka 16 wanawake kabla masharti yao kuzingatiwa.

Msemaji wa kundi la Taliban, Qari Mohammed Yousuf, amesema serikali haijawasiliana nao tangu kiongozi wa kundi hilo alipotangaza jana kwamba litaanza kuwaua mateka hao kuanzia saa sita leo mchana.

Aidha amesema kundi la Taliban halitabadili msimamo wake kuhusu mateka hao wa Korea Kusini.