1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kabul. Mateka kuachiliwa huru.

13 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBZm

Gavana wa jimbo la Ghazni amesema kuwa mateka wawili wanawake wa Korea ya kusini wanaoshikiliwa na wanamgambo wa Taliban huenda wakaachiliwa katika saa chache zijazo.

Gavana Merajuddin Pattan amekuwa katika kikao juu ya mazungumzo yenye lengo la kujadili kuachiliwa kwa mateka 21 waliobaki wa Korea ya kusini. Taliban tayari wamewauwa mateka wanaume wawili na kutishia kuwauwa wengine wote hadi pale wafungwa wa Taliban walioko gerezani watakapoachiliwa huru kwa kubadilishana na mateka hao.

Serikali ya Afghanistan imekataa kukubali madai ya wateka nyara hao.