1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KABUL: Maafisa watano wa polisi wauwawa kimakosa

16 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCIT

Serikali ya Afghanistan inasema wanajeshi wa muungano wanaoongozwa na Marekani nchini humo wamewaua polisi watano wa Afghanistan kimakosa kwenye tukio lililotokea katika mkoa wa Helmand kusini mwa nchi hiyo.

Jeshi la Marekani nchini Afghanistan limeknusha madai hayo. Msemaji wa jeshi la muungano nchini Afghanistan, sajini Dean Welch amesema uchunguzi unaendelea kubaini kilichotokwa na waliohusika katika kisa hicho.

Msemaji wa serikali ya Afghanistan amesema polisi hao walikuwa wakishika doria kwenye kituo cha upekuzi katika wilaya ya Gereshk mkoani Helmand jana jioni wakati majeshi ya muungano yalipowashambulia kwa risasi kimakosa.

Tukio hilo limefanyika huku majeshi ya shirika la NATO nchini Afghanistan yakiendelea na operesheni yao kujaribu kuudhibiti mkoa wa Helmand ambao ni ngome ya waasi wa Taliban.

Wakati huo huo, waasi wa Taliban wamemuua dereva wa mwandishi wa habari mtaliani, Daniele Mastrogiacomo, lakini wameahirisha kumuua mwandishi huyo mpaka Jumatatu ijayo.