KABUL : Kansela Merkel afanya ziara ya ghafla Afghanistan | Habari za Ulimwengu | DW | 03.11.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

KABUL : Kansela Merkel afanya ziara ya ghafla Afghanistan

Kansela Angela Merkel wa Ujerumani amefanya ziara ya ghafla nchini Afghnaistan.

Kutokana na sababu za kiusalama ziara yake imefanywa kuwa siri hadi dakika za mwisho.Merkel anatazamiwa kukutana na Rais Hamid Karzai kujadili hali ya usalama katika nchi hiyo ilioathiriwa na vita.Baadae atakaguwa kikosi cha Ujerumani kilioko nchini humo.

Mwezi uliopita bunge la Ujerumani limeidhinisha kuongeza muda shughuli za kijeshi za Ujerumani nchini Afghanistan wakati uungaji mkono wa wananchi kwa shughuli hizo ukizidi kupunguwa.

Kuna takriban wanajeshi 3,000 wa Ujerumani waliowekwa kaskazini mwa Afghanistan kwenye kikosi cha Usaidizi cha Kimataifa kinachoongozwa na Umoja wa Kujihami wa Mataifa ya Magharibi NATO.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com