1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KABUL: Kamanda mkuu wa kundi la Taliban auawa.

4 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCV8

Majeshi ya NATO yamesema yamemuuwa kamanda wa kundi la Taliban katika eneo la kusini mwa Afghanistan kwenye mapigano ya kujaribu kutwaa tena udhibiti wa mji uliotekwa na wanamgambo hao.

Kwa mujibu wa majeshi hayo, kiongozi huyo wa Taliban, Mullah Ghafour, aliuawa baada ya gari lake kushambuliwa kutoka hewani karibu na mji wa Musa Qala katika jimbo la Helmand.

Wanamgambo wengine kadhaa wa Taliban wanasemekana waliuawa.

Shambulio hilo limetekelezwa wakati ambapo Marekani leo inachukua zamu yake ya uongozi wa kikosi hicho cha NATO ambacho kina wanajeshi elfu thelathini na tatu.