KABUL: Kaburi la umma lagunduliwa Afghanistan | Habari za Ulimwengu | DW | 06.07.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

KABUL: Kaburi la umma lagunduliwa Afghanistan

Kaburi la mamia ya watu,limegunduliwa katika jela ya chini kwa chini,kaskazini ya mji mkuu wa Afghanistan,Kabul.Kaburi hilo limegunduliwa katika kituo cha kijeshi kilichokuwa kikitumiwa wakati wa uvamizi wa Soviet Union ya zamani. Mwanamume mwenye umri wa miaka 70 alierejea Afghanistan,aliwaonyesha maafisa kaburi hilo la umma,ikisemekana kuwa wahanga hao walijengewa ukuta wakiwa hai.Zaidi ya Waafghanistan milioni 1.5 waliuawa na maelfu wengine ama waliteswa au walibakwa,wakati wa mapigano ya kupinga uvamizi na katika vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyofuata.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com