Kabul: Inadaiwa Helikopa ya Kimarenai imedenguliwa huko Afghanistan
18 Februari 2007Matangazo
Jeshi la Muungano linaloongozwa na Marekani huko Afghanistan limesema moja ya helikopta zake imeanguka kusini mashariki ya nchi hiyo. Katika taarifa, jeshi la Marekani lilisema wanajeshi wanane waliuwawa na 14 walijeruhiwa katika ajali hiyo, baada ya rubani kuripoti kwamba injini ya helikopta hiyo ilikuwa ina matatizo. Wapiganaji wa Taliban wanadai wameidungua helikopta hiyo kwa kutumia roketi.