KABUL: Hakuna maendeleo kuhusu mateka nchini Afghanistan | Habari za Ulimwengu | DW | 05.08.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

KABUL: Hakuna maendeleo kuhusu mateka nchini Afghanistan

Ubalozi wa Korea ya Kusini katika mji mkuu wa Afghanistan,Kabul umethibitisha kuwa yalikuwepo mawasiliano pamoja na wateka nyara wa raia 21 wa Korea ya Kusini.Wakati huo huo,Korea ya Kusini inatumaini kuwa majadiliano kati ya Rais wa Marekani George W.Bush na Rais Hamid Karzai wa Afghanistan alie ziarani Marekani,yatakuwa na matokeo mazuri.

Hapo awali,Rais Karzai alisema,kinachotakiwa ni kuachiliwa huru kwa usalama Wakorea waliozuiliwa na magaidi nchini Afghanistan.Akaongezea kuwa magaidi hao wana asili ya kigeni lakini Afghanistan inapata sifa mbaya kwa vile kitendo hicho kimetokea nchini Afghanistan.

Hii leo,Karzai anakutana na Bush na inatazamiwa kuwa mada kuu itahusika na utekaji nyara wa raia 21 wa Korea ya Kusini na mhandisi wa Kijerumani.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com