KABUL: Hakuna kipya kuhusu hatima ya mateka | Habari za Ulimwengu | DW | 28.07.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

KABUL: Hakuna kipya kuhusu hatima ya mateka

Hatima ya mhandisi wa Kijerumani alietekwa nyara nchini Afghanistan,zaidi ya juma moja lililopita, bado haijulikani.Wizara ya mambo ya nje ya Ujerumani,mjini Berlin imesema,kikundi maalum cha dharura kinaendelea na juhudi zinazohusika na kuachiliwa huru mhandisi huyo.Msemaji wa wizara hiyo lakini,alikataa kutoa maelezo zaidi. Mjerumani mwengine alietekwa nyara Afghanistan pamoja na mhandisi huyo,alifariki alipokuwa amezuiliwa mateka.Maiti yake imeletwa Ujerumani mapema juma hili.Madaktari wanaochunguza maiti hiyo wamesema,itachukua muda wa siku kadhaa kugundua kile kilichosababisha kifo cha mateka huyo.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com