KABUL: Askari 6 wa NATO raia wa Canada wauwawa | Habari za Ulimwengu | DW | 05.07.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

KABUL: Askari 6 wa NATO raia wa Canada wauwawa

Takriban wanajeshi sita raia wa Canada na mkalimani wao wameuwawa nchini Afghanistan katika shambulio la bomu la kutegwa kando ya barabara.

Bomu hilo lilipua gari la kikosi hicho cha NATO katika jimbo la Kandahar, kusini mwa Afghanistan.

Vifo hivyo vimeongeza idadi ya wanajeshi wa kigeni waliouwawa mwaka huu na kufikia 102.

Wakati huo huo wizara ya mambo ya nje ya Ujerumani imefahamisha juu ya kutoweka raia wa Ujerumani nchini Afghanistan tangu alhamisi iliyopita.

Polisi nchini Afghanistan imesema kwamba itakutana na watekaji nyara kutathmini sababu za kutekwa nyara injinia huyo raia wa Ujerumani ambae inaaminika kuwa hakutekwa nyara na wanamgambo wa Taliban bali na kundi la majambazi.

Hii ni mara ya kwanza kwa raia wa Ujerumani kutekwa nyara nchini Afghanistan tangu kuangushwa kwa utawala wa Taliban mnamo mwaka 2001.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com