KABUL: Afisa mmoja wa polisi auwawa
23 Mei 2007Matangazo
Afisa mmoja wa polisi ameuwawa wakati mshambuliaji wa kujitoa muhanga maisha aliyekuwa kwenye pikipiki alipojilipua karibu na makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini Kabul. Watu wengine watano wamejeruhiwa kwenye shambulio hilo, wakiwemo maafisa wawili wa polisi.
Msemaji wa polisi amesema hujuma hiyo imefanywa katika mojawapo ya barabara zilizo na shughuli nyingi mjini Kabul.