Kabila aitembelea Congo Brazzaville | Matukio ya Kisiasa | DW | 04.06.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Kisiasa

Kabila aitembelea Congo Brazzaville

Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo na mwenziye Dennis Sassounguesso wa congo Brazzaville wamehakikisha nia yao ya kurejesha amani na kuboresha uhusiano kati ya DRC na Kongo Brazzaville.

Joseph Kabila

Joseph Kabila

Rais Joseph Kabila amewataka wanamgambo wote walioko mashariki mwa nchi yake watue chini silaha na ameahidi kurejesha amani na usalama kabla ya mwaka huu kumalizika. Aliyasema hayo wakati waziara yake ya siku mbili mjini Brazzaville.

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com