1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Jumuiya ya Afrika Masharika yakua

18 Juni 2007

Viongozi kutoka Jumuiya ya Afrika Mashariki wako mjini Kampala nchini Uganda kuwajumuisha rasmi mataifa ya Rwanda na Burundi. Jumuiya hiyo sasa ina nchi tano wanachama.

https://p.dw.com/p/CB3X

Marais hao wanatarajiwa kuzindua rasmu wimbo wa Jumuiya ya Afrika Mashariki vilevile kumuapisha Julias Tangus Rotich makamu mpya wa Katibu Mkuu. Aidha rais Yoweri Museveni wa Uganda anapokea rasmu uwenyekiti wa Jumuiya hiyo kutoka kwa Rais Mwai Kibaki wa Kenya.

Rwanda na Burundi zilijiunga na Jumuiya hiyo mwezi Novemba mwaka jana na kusubiri uanachama kamili kuanza mwezi Julai.