Jumuia ya SADC yakutana kesho
29 Machi 2009Matangazo
Mbabane:
Viongozi wa jumuia ya maendeleo kusini mwa Afrika-SADC wanakutana kesho kwa mkutano wa dharura kuzungumzia uwezekano wa kuwekewa vikwazo viongozi wa kipindi cha mpito kisiwani Madagascar na rais wao Andry Rajoelina."Viongozi wa SADC watatathmini njia za kurejesha demokrasia,na taifa linaloheshimu sheria na katiba kisiwani Madagascar" imesema serikali ya Afrika kusini-Mwenyekiti wa sasa wa jumuia hiyo ya kimkoa."Viongozi wa mataifa yote wanachama wameahidi watahudhuria mkutano huo"imesema kwa upande wake wizara ya mambo ya nchi za nje ya Swazilanz.Haikutajwa lakini viongozi gani wa Madagascar wamealikwa mkutano huo.SADC inapinga kuutambua utawala mpya unaoongozwa na Andry Rajoelina kisiwani Madagascar.