Jukwaa la uchumi.
12 Juni 2009Wajumbe zaidi ya 600 wanakutana kwenye Jukwaa,la uchumi mjini Cape Town kujadili njia za kukabiliana na mgogoro mkubwa wa uchumi ulioikumba dunia.
Wajumbe hao kutoka duniani kote wanaowakilisha sekta za uchumi na siasa wanajadili hali ya uchumi ya bara la Afrika katika mazingira ya mgogoro mkubwa wa uchumi. Jukwaa hilo limehutubiwa pia na mwenyeji, rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini na rais Paul Kagame wa Rwanda.
Wajumbe hao wanajadili njia za ufanisi za kukabiliana na mgogoro wa uchumi. Mgogoro huo unatishia kuvuruga ustawi wa uchumi uliofikiwa katika nchi za Afrika za kusini mwa jangwa la Sahara.
Rais Zuma amezilaumu nchi tajiri kwa kuweka vizingiziti katika biashara kinyume na ahadi zilizotoa juu ya kurahisisha uhusiano wa kibiashara na nchi za Afrika.
Akizungumza kwenye kongamano hilo rais Paul Kagame wa Rwanda amezitaka nchi za Afrika ziache tabia ya kusubiri waokozi kutoka nje ili waje kutatua matatizo ya Afrika.Amesema Afrika inapaswa kutatua matatizo yake kwa kutumia nguvu zake.
Kutokana na mgogoro wa uchumi waekaji vitega uchumi kutoka nje wamepungua barani Afrika.Mabenki yanabania mikopo kwa wajasiramali wadogo wadogo .
Wajumbe kwenye jukwaa la uchumi mjini Cape Town wanajadili njia za kukabiliana na matatizo hayo.
Mwandishi/AbdulMtullya
Mhariri/M.Abdul-Rahman