Jukwaa la Manufaa2 | NRS-Import | DW | 29.11.2011
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

NRS-Import

Jukwaa la Manufaa2

Ni wasaa wa kesema chochote cha msingi katika jukwaa la manufaa, karibia usike yako lakini pia hata maneno mengine kutoka kwa wasikilizaji wengine kutoka maeneo tofauti. Jina langu Sudi Mnette.

Wer hat das Bild gemacht/Fotograf?: Chameleonseye Wann wurde das Bild gemacht?: 2008 Wo wurde das Bild aufgenommen?: Gebetsplatz Bildbeschreibung: Muslime beim Gebet Copyrightangabe: ©chameleonseye.com – Fotolia.com

Waislam

Muzik

Sauti sa

Naaza kwa nukuu"Siku zote watazamani wa mpira ndio wanaojua kucheza zaidi ya wale waliyoko uwanjani, watu wanafikiri kuongoza nchi ni lelemama, kila mtu anaweza, yapo mapungufu ya viongozi wetu na lazima wajirekebishe, heri aliyekula kidogo na akatulia kuliko yule mwenye uchu na njaa kali, hamjui akiingia madarakani atakula kwa staili gani, hakuna nchi inayoongozwa na malaika, wote ni binadamu kama mimi na wewe. si maneno yangu bali ni James masawe wa Tanga Tanzania, bila shaka hapo Masawe ana yake moyoni na hasa kufutia hali ya kisiasa kwa hivi sasa nchini humo lakini hapo anatumia utajiri wake wa Kiswahili.

Stimmung in Marokko nach dem WahlSieg von Islamisten Partei Main title: marwa talal Photo title: Morocco/ elections/reaction of a young moroccan woman 27.11.2011 Kopierechte von Siham Ouchtou, DW arabisch Korrespondentin in Marokko. Zugestellt von Moncef Slimi

Mwanamke

Na sasa ni nafasi ya Calist Tesha kutoka huko huko Tanga akisema, serikali ya Kenya inajitahidi kuleta usalama nchini Somalia kwa sababu al-Shabaab wanatishia ustawi wa uchumi wa Kenya na eneo zima la Afrika Mashariki. Tesha anaongeza kwa kusema kundi hilo la kigaidi hatari yake ipo hata katika usafiri wa baharini. Kwa hiyo kupeleka Kenya kupeleka jeshi Somalia ni kitendo cha ushujaa na kiungwana. Aidha Calist amezitaka nchi nyingine kuiga mfano huo.

Tukitoka Tanga tunakwenda moja kwa moja nchini Zambia, huko tunakutana na Dk. Gary Wakigana Mikalamo yeye anasema " Mimi napenda tena jukwaani leo,kwa kuwaambia tu ndugu zangu wa Congo kwama unapaowadia wakati wa uchaguzi sio wakati wa vurugu. Kila mtu ana nafasi ya kuchaguliwa kama wafanyavyo wachezaji wa mpira, kila mmoja anaisi atashinda. lakini kubwa mara nyinge katika chaguzi waige mfano wa Zambia.

Nae Zoka Paul Mabusi, huyu mimi namwita mzee wa busara hapa anatoa wito kwa watu wote kukumbuka kuwasaidia watu mbalimbali bila ya kutegemea malipo yeyote kutoka kwao. Zoka anawakumbusha mnetembelee yatima, wafungwa, wagonjwa, yatima na wajane.

Na sasa nakamata barua yake Salome Lufunda kutoka Chuo cha Sebastian Kalowa huko Tanga akisema Tanzania ipo katika harakati za kilimo kwanza. Kauli hiyo inamtaka Mtazania kuchangia chochote kwa kadiri awezavyo katika kilimo.

Leo hii Salome anatoa elimu ya kilimo cha matunda.

Anaanza kwa kusema" Kuna mimea ya aina nyingi matunda za matunda Tanzania kama vile michungwa, miembe, minanasi, mipapaim nigomba mipera, miparachichi, mibohora, mlakwati mtomasi, mitofaa, mipea, miplamu, mizabibu,

katika somo lake hili Salome anasema mimea hiyo inaweza kumea katika maeneo tofauti na mikoa yote ya Tanzania. Matunda ni chakula na kimo katika orodha ya vyakula vilivyotiliwa mkazo. Lakini pia pamoja na kuhimza Watanzania kushiriki kilimo hicho amesema matunda yanaweza kuongeza kipato.

Ni Maneno yaliyo katika barua ya Salome akihimiza kilimo kwanza kwa Watanzania wenzake.

Na sasa Filbert Kyauke wa Mlandizi Tanzania anapanda jukwaani kwa kuzungumzia tatizo la kutupa taka ovyo, anasema utupaji taka ovyo limekuwa jambo la kawaida kwa wakazi wa mji wa Mlandizi. kutokana na tatizo hilo Kyauke alihoji hao wanaofanya vitendo hivyo wananufaika na nini? hata hivyo Kyauke hakuishia hapo bali alihimiza serikali kuchukua hatua kali dhidi ya wanaofanya vitendo hivyo.

Na sasa naikamata barua ya Fikiri Dariro akihimizwa wananchi wa Tanzania wasiburuzwe katika suala la katika lazima kwa namna yeyote kila mtu ahakikishe anashiriki katika kufanikisha katiba bora na yenye tija katika taifa. Fikiri anasema Wananchi wanapaswa kushiriki katika mchakato wa katiba mpya kama ilivyo katika uchaguzi.

Katika barua yake Amosi Msanga kutoka Ludewa anazungumzia mmomonyoko wa maadili. yeye anasema anakerwa sana na vitendo vya ukahaba, mavazi mafupi na ya kubana. kutokana na hali hiyo anahimiza vyombo vya sheria visinyamaze kimya.

Msikilizaji anaetusha kutoka jukwaani kwa leo hii ni Henry Kideula wa Njombe Tanzania anaesema nchi yake ina maeneo mengi yanayoweza kuwavutia wawekezaji wa ndani na nje, lakini kwa kipindi kirefu imegundulika kuwa baadhi ya wawekezaji sio waaminifu. Henry anasema mara kadhaa kumekuwa na ripoti za wawekezaji hao kukiuka mikataba na kufanya biashara nyingine tofauti na makubaliano ya msingi. Hali hiyo imesababisha fursa nyingi ikiwemo ya watu kupoteza nafasi ya ajira na fursa ya pato litokanalo na uwekezaji husika. Kutokana na hali hiyo Henry anashauri serikali kufanya uchunguzi wa kina na kuendelea kufanya ukaguzi kila wakati ili kuweza kudhibiti hali hiyo.

" Ama kweli dunia ya kale si ya sasa, zamani tulikuwa tukihadithiwea na mababu, hadithi zilizohusu ushujaa wa kuwinda na kuwauwa wanyama wakali kama simba, chui, tembo na wengine wengi tu. Cha ajabu watu hawana haja na wanyama tena isipokuwa binadamu wanawindana sana. Kama si kwa panga, kwa mkuki, kama si kwa mkuki mabomu na bunduki, kama haitoshi kwa uchawi na kudhulumu mali za wengine hasa wanyonge. Wengi ni mashahidi hata Gaddafi amewindwa kama mnayama pori anaekula maboga ya bibi, hali watanzania tufunge na kuomba kwani uwezekano wa kutokea upo" hayo ni maneno ya Amos Msanga.

Msikilizaji, kwanza nashukuru kuwa nawe kwa muda wote lakini pia niseme kwa heri na indelelea kusikiliza DW , kipindi jukwaa la manufaa mie nilikuwa Sudi Mnette

Mwandishi: Sudi Mnette

Mhariri:

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com