Joto la uchaguzi mkuu linazidi nchini Kenya
20 Septemba 2007Matangazo
Mwenyekiti wa chama cha Kaddu na mshirika wa karibu wa rais wa zamani Daniel Arap Moi na pia aliyewahi kuwa waziri katika utawala wa Moi Cyrus Jirongo ametangaza kumuunga mkono mgombea wa chama cha ODM Raila Odinga hatua ambayo inatofautiana na ile ya rais Kibaki.
Katika chama cha ODM kenya Kalonzo Musyoka amemteua Julia Ojiambo kuwa mgombea wake mwenza huku kukiwa na habari kwamba juhudi zinaendelea kuzitaka ODM mbili kufikia muafaka wa ushirikiano kuimarisha nguvu za upinzani kukabiliana na raia Kibaki.
Saumu Mwasimba alizungumza na Julia Ojiambo na kwanza akieleza juu ya hisia zake baada ya kuteuliwa kuwa mgombea mwenza wa Kalonzo Musyoka.