1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Joseph Kabila kuapishwa rais wa DRC kwa muhula mwingine

Martin,Prema/zpr20 Desemba 2011

Hali ya wasiwasi imezuka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, ambako kiongozi wa upinzani Etienne Tshisekedi anashikilia kuwa yeye ndio alie na haki ya kutangazwa rais kufuatia uchaguzi wa Novemba 28.

https://p.dw.com/p/13VrP
Provisional results show Joseph Kabila as winner of Congo preside epa03029391 (FILE) A file picture dated 24 October 2011 shows Joseph Kabila, President of the Democratic Republic of Congo, looking on, during the closing news conference at the Francophone Summit in Montreux, Switzerland. Incumbent Joseph Kabila was on 09 December 2011 declared the winner of last month's presidential elections in the Democratic Republic of Congo, defeating 10 other candidates, according to the country's election commission. The results still need to be confirmed by the supreme court. According to media reports on 09 December 2011, opposition leader Etienne Tshisekedi has declared himself president, only a few hours after hours after provisional results shows that Joseph Kabila had won. EPA/DOMINIC FAVRE *** Local Caption *** 00000402410042
Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Joseph KabilaPicha: picture alliance/dpa

Tshisekedi anashikilia hivyo, licha ya mahakama kuu nchini humo siku ya Ijumaa kuthibitisha kuwa rais wa sasa Joseph Kabila ameshinda kwa kupata asilimia 49 ya kura na Tshisekedi asilimia 32.

Umoja wa Afrika umeueleza uchaguzi huo kama ni mafanikio, lakini Umoja wa Ulaya, Kituo cha Carter chenye makao yake nchini Marekani na wasimamizi wengine wa uchaguzi wanasema, uchaguzi wa Novemba 28 ulikuwa na dosari.

Joseph Kabila anatazamiwa kuapishwa leo kwa awamu nyingine. Tshisekedi pia amejipangia sherehe ya kuapishwa siku ya Ijumaa.