JOHANNESBURG : Majirani wa Zimbawe ni sehemu ya tatizo | Habari za Ulimwengu | DW | 10.03.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

JOHANNESBURG : Majirani wa Zimbawe ni sehemu ya tatizo

Kiongozi wa upinzani nchini Zimbabwe Morgan Tsvangirai amezishambulia nchi za kusini mwa Afrika kwa kuwa sehemu ya tatizo la kisiasa na kiuchumi la Zimbabwe.

Kauli yake hiyo inaonekana kukususia kukataa kwa Afrika Kusini kusaidia kukomesha mgogoro uliko katika nchi jirani yake.

Tsvangirai kiongozi wa chama cha upinzani cha Vuguvugu la Mabadiliko ya Kidemokrasia MDC ameuambia mkutano wa kila mwaka wa chama cha waandishi wa habari wa kigeni mjini Johnnesburg kwamba badala ya kuwa sehemu ya utatuzi wa mzozo huo nchi za Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika SADC zimekuwa sehemu ya tatizo hilo.

Afrika Kusini ni taifa lenye nguvu kubwa za kiuchumi katika jumuiya ya SADC na Rais wake Thabo Mbeki anaonekana kuwa kiongozi wa Afrika mwenye ushawishi zaidi kwa Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe.

Tsvangirai amesema nchi hizo zimekuwa zikimuunga mkono Mugabe kimya kimya katika masuala ambayo wanajuwa kuwa hayuko sawa.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com