1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Jinsi gazeti la Bild linavyomtetea waziri wa ulinzi

25 Februari 2011

Eti ajiuzulu kwasababu ya kutumia maelezo ya watu bila ya kuwataja majina katika mtihani wa shahada ya udaktari-PHD au la?Hilo ndilo suala linalo yagonganisha vichwa magazeti humu nchini.

https://p.dw.com/p/10PKQ
Waziri wa ulinzi Karl-Theodor zu GuttenbergPicha: dapd

Kisa cha waziri wa ulinzi wa serikali kuu ya Ujerumani ,mwanasiasa anaependwa zaidi humu nchini,Karl-Theodor zu Guttenberg cha kutumia maelezo ya watu katika shahada yake ya udaktari (PHD) tena bila ya kuwataja kinazidi kuhanikiza. Katika vyombo vya habari mengi yamekuwa yakiandikwa kuhusu kisa hicho. Kauli mbiu katika vyombo vya habari ni moja tuu: zu Guttenberg cheo chake amekipata kwa njia za udanganyifu kwa hivyo lazma ajiuzulu. Gazeti moja ndilo linalomtetea kwa nguvu waziri wa ulinzi: Gazeti la mitaani linalosomwa kila siku na mamilioni ya wajerumani-"Bild".

February 16, gazeti la Süddeutsche Zeitung lilikuwa gazeti pekee lililoripoti kuhusu maelezo yasiyolingana katika mtihani wa shahada ya udaktari (PHD) ya Karl-Theodor zu Guttenberg. Dhana za kutumia maelezo ya watu bila ya kuwataja-ndio iliyokuwa mada kuu iliyochambuliwa katika ukurasa wa pili wa gazeti hilo linalosomwa na wengi katika kila pembe ya Ujerumani. Hapajapita muda magazeti yote yakaanza kuripoti kuhusu kashfa hiyo.

Sonntagszeitung Bild am Sonntag
Bibi mmoja anasoma gazeti la Bild, toleo la jumapiliPicha: picture-alliance/dpa

Bila ya shaka gazeti kubwa kabisa la mitaani barani Ulaya halijaweza kuipuuza kadhia hiyo; hata hivyo lilijizuwia kidogo. "Vurugu kuhusu shahada yake ya udaktari" ndio kilichokuwa kichwa cha maneno" maneno yaliyoandikwa kwa herufi ndogo ambazo hazilingani na utaratibu wa maandishi wa gazeti la Bild katika ukurasa wake wa kwanza.

Kwamba gazeti hilo mashuhuri linalomilikiwa na shirika la uchapishaji la kihafidhina "Axel Springer", linamtetea waziri huyo aliyeingia midomoni, msomaji hajakosa kutambua hali hiyo katika ukurasa wa pili pale mwandishi wa makala maalumu katika gazeti hilo Franz-Josef Wagner alipoandika makala yake aliyoipa jina "Mpendwa Dr. zu Guttenberg." na kuendelea kuandika tunanukuu:"

"Sijui chochote kuhusu namna ya kuandika shahada ya udaktari (PHD). Nimefeli mtihani wa kidato cha sita na sijawahi hata siku moja, kuingia ndani katika chuo kikuu. Kutoka nje ninaweza kusema: Usimsumbuwe bure mtu huyo mzuri. Sahau cheo cha udaktari."

Hiyo ni lugha halisi inayotumiwa na gazezi la Bild. Wanaochangia katika gazeti hilo wanajitaja kuwa "mawakili wa wasiokuwa na sauti". Na kuhusiana na kisa cha zu Guttenberg ni dhahiri kabisa -mwanasiasa huyo ni kipenzi cha umma. Muhimu zaidi lakini ni kwamba waziri wa ulinzi tangu mwanzo alijitahidi kuelemea upande wa gazeti la Bild na akafanikiwa. Naiwe kikazi au kibinafsi, mara zote amekuwa akisikilizwa.

Deutschland Plagiats-Affäre Karl-Theodor zu Guttenberg Doktorarbeit und Buch vom Großvater
KItabu"Fussnoten" kilichoandikwa na babu yake Karl Theodor zu Guttenberg kati ya mwaka 1921-1972Picha: dapd

Ikiwa mwanasiasa huyo anafanya ziara ya ghafla nchini Afghanistan kuwazuru wanajeshi wa Ujerumani, basi ripota wa gazeti la Bild daima huwa miongoni mwa waandishi habari wachache wanaoteuliwa kufuatana naye.

Na hata kuhusu harakati za mkewe Stefanie ambaye anaendesha vipindi vya televisheni ya kibinafsi kuhusu mapambano dhidi ya wahalifu wanaowabaka na kuchafua hadhi ya watoto, zinachambuliwa kikamilifu na gatezi hilo la Bild.

Nikolaus Blome, anayeongoza makao makuu ya gazeti la Bild mjini Berlin anazungumzia msimamo wa shirika lake kuhusu kipindi cha televisheni cha "Hart aber Fair" na kusema:

"Ukweli ni kwamba tuna maoni yetu kuhusiana na waziri huyo na tunamuona ni mzuri. Na wanaomuonea wivu, wanaonung'unika na wanaomfuja..... Hayo watu wameshayazoweya."

Hapo Blome anamaanisha waandishi habari wanaohoji zu Guttenberg anabidi ajiuzulu.

Mwandishi:Fürstenau,Marcel (DW Berlin)neu/Hamidou Oummilkheir

Mhariri:Josephat Charo