1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Jeshi la Uturuki lashambulia Iraq kaskazini

11 Januari 2008
https://p.dw.com/p/CoSX

ARBIL, Iraq

Jeshi la Uturuki limeshambulia kwa mizinga maeneo yanayotuhumiwa kwa ya waasi wa Kikurdi kaskazini mwa Iraq.

Afisa wa serikali ya mamlaka ya ndani ya Wakurdi kaskazini mwa Iraq amesema mashambulizi hayo ya mizinga yamelenga maeneo mawili katika jimbo la Dahuk kwa takriban masaa mawili. Hakuna taarifa zilizoweza kupatikana mara moja juu ya maafa.

Hili ni shambulio la kwanza la kuvuka mpaka kuwahi kurepotiwa tokea shambulio la bomu la Januari tatu ambalo limeuwa watu sita katika mji wa kusini mashariki wa Uturuki wa Diyarkabir ambapo serikali ya Uturuki imesema waasi wa Kikurdi walihusika na shambulio hilo.