1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUkraine

Jeshi la Ukraine lakabiliwa na hali ngumu

10 Januari 2024

Jeshi la Ukraine limesema vikosi vyake vya ardhini vinaendelea kukabiliana na mashambulizi ya Urusi licha ya baridi kali na kwamba hapo jana wamefanikiwa kuzima jumla ya mashambulizi ya urusi 64.

https://p.dw.com/p/4b2pU
Ujerumani | Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky ziarani katika kambi ya Wiesbaden
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky (aliyetia mkono kifuani) alipotembelea kambi ya jeshi la Marekani huko Wiesbaden nchini Ujerumani (14.12.2023)Picha: Ukraine Presidency/ZUMA/picture alliance

Rais Volodymyr Zelensky amesema wanahitaji kuongeza kasi ya usambazaji wa vifaa kama droni kwa wapiganaji walio katika mstari wa mbele wUkraine inafikiria kuhamasisha watu 500,000 zaidi wajiunge na jeshi katika vita vyake na Urusia vita huku akikiri kuwa wanajeshi wake wanakabiliwa na uhaba wa risasi.

Leo Jumatano, wajumbe wa  Baraza la pamoja la Jumuiya ya kujihami NATO na Ukraine  watakutana mjini Brussels nchini Ubelgiji ili kujadili ongezeko la hivi karibuni la mashambulizi ya Urusi dhidi ya Ukraine ambayo yamesababisha vifo vya makumi ya watu.