Jeshi la Uingereza laanza kuondoka katika mji wa Basra
3 Septemba 2007Matangazo
Vikosi vya Uingereza vilianza kuondoka kutoka mji wa Basra kusini mwa Irak kuanzia jana usiku katika hatua ya kukabidhi mamlaka kwa vikosi vya Irak huku Uingereza ikijitayarisha kuviondoa vikosi vyake kutoka nchini Irak. Wizara ya Ulinzi ya Uingereza imesema kwamba maafisa wa Marekani walifahamishwa juu ya kuondoka kwa vikosi hivyo vya Uingereza kutoka mji wa Basra.
Wakati huo huo jemadari mwingine aliyestaafu wa jeshi la Uingereza amekosoa mkakati wa Marekani nchini Irak.
Katika mazungumzo na gazeti la jumapili la nchini Uingereza la SUNDAY MIRROR meja jenerali Tim Cross ameieleza sera ya Marekani nchini Irak kuwa imeshindwa kabisa kufaulu.
Meja jenerali Cross alikuwa afisa wa ngazi ya juu katika jeshi la Uingereza.