1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Jeshi la Pakistan

18 Februari 2008

Jeshi la Pakistan ni dola ndani ya dola ?

https://p.dw.com/p/D9K8

Dola ndani ya dola ndivyo jeshi linavyoelezwa nchini Pakistan:

swali jeshi hili litachukua msimamo gani siku za usoni nchini Pakistan ambako jana ulifanyika uchaguzi uliogubikwa na kamepni dhidi ya jamadari Musharraf na kuuwawa kwa Benazir Bhutto wa Pakistan Proples' party.

Jeshi la Pakistan lina jumla ya askari milioni 1.4 na linakula 20% ya bajeti nzima ya Pakistan.

Ikiwa kuna yeyote ambae daima ana sauti katika pakistan basi ni jeshi la nchi hiyo.Jeshi la pakistan lina askari milioni 1.4 na linam,eza 20% ya matumizi ya serikali na kwa wapakistan wengi,jeshi lao ni dola ndani ya dola.ndio maana linachomoza swali hili:jeshi hili katika siasa uza Pakistan siku za mbele litachukua msimamo gani ?

Na hasa wakati huu ambao ushawishi na nguvu za waislamu wenye itikadi kali unaongezeka humo nchini.

"Tunaupinga utawala huu.Vita vetu dhidi ya serikali hii vitaendelea."

Hivyo ndivyo alivyonadi Abdul Rashid Ghazi kiongozi wa waumini hao wenye itikadi kali katika msikiti mwekundu wakati wa mazungumzo ya simu .Haukupita muda Rashid Ghazi aliuwawa tena si pekee yake bali na wenzake msikitini.Alikuwa rais jamadari Musharraf alipeleka askari wake kupambana nao msikitini.

Vita vya kupambana na ugaidi havikumalizikia hujuma hii ya kijeshi.Tumevinjari kuwahilikisha magaidi kokote waliko,katika kila mkoa na kila pembe ya nchi hii."

tangu wakati huo kumeibika mashina kadhaa ambako magaidi hao ndio wenye usemi na hadi karibuni hivi kwa muujibu asemavyo bingwa wa maswali ya kijeshi wa kipakistan Hassan Askari Rizvi:

"Kuna watu serikalini na jeshini wanaowaungamkomno magaidi hao .Serikali haikua na azma ya kuwatimua watu kama hao.Ikidhani huenda siku moja ikawahitaji.Lakini tangu pale watu hawa wanasababisha udhia kwa serikali ya Pakistan,siasa imebadilika."

Labda wamechelewa sasa kuwachukulia hatua.Kwani pale jamadari musharraf alipotekeleza mojawapo ya ahadi zake na akavuja mavazi yake ya kijeshi katika sherehe hiyo maalumu, hakuna tena alimuamini.hii ni kwa sababu alikwishatangaza hali ya hatari ili kuwapiga vita magaidi pamoja pia na wakosoaji serikali yake aliowatia nguvuni wakijumuisha mahakimu na mawakili.Wapakistan wengi hawamtaki tena jamadari musharraf akiwa mwanajeshi au bila kuwa mwanajeshi wamechoka nae.

Bingwa mmoja Shafqat Mahmood anasema kwavile jeshi lilimuungamkono jamadari musharraf kwa miaka 8,hata nalo limepoteza imani ya wananchi.Na hii haiwapendezi majamadari na ndio maana anadai bingwa Hassan Askari jeshi sasa linataka kujitoa katika siasa.

Jeshi nchini Pakistan lina turufu kubwa:laweza ama kuiungamkono serikali au kuiangusha.Lina mkono wake pia katika uchumi.