Jeshi la Israel lashambulia maeneo ya Gaza | Habari za Ulimwengu | DW | 06.01.2008
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Jeshi la Israel lashambulia maeneo ya Gaza

Jerusalem:

Jeshi la Israel limeivamia kambi ya wakimbizi ya El Boureij katika ukanda wa Gaza na helikopta za kivita kuvurumisha mizinga mara mbili katika ardhi hiyo ya wapalastina.Mpalastina zaidi ya mmoja ameuliwa na wengine kujeruhiwa.Duru za Palastina zinasema madege ya kivita ya Israel yamehujumu pia Beit Hanoun.Akihojiwa na shirika la habari la Ufaransa AFP,msemaji wa kijeshi wa Israel amedhibitisha opereshini za kijeshi zinaendelea katika ukanda wa Gaza.Hapo awali maelfu ya waisrael wenye asili ya kiarabu waliandamana kwa amani katika mji wa kaskazini wa Israel Nazareth kudai Israel iache kulizingira eneo la Gaza.Israel imeliwekea vikwazo eneo la Gaza tangu mwezi June uliopita,baada ya Hamas kulidhibiti eneo hilo.Wakati huo huo duru za kuaminika zinasema waziri mkuu wa Israel Ehud Olmert huenda akakutana na kiongozi wa utawala wa ndani wa Palastina Mahmoud Abbas kabla ya ziara ya rais George W. Bush wiki ijayo.Viongozi hao wawili walikutana kwa mara ya mwisho December 27 iliyopita mjini Jerusalem.

 • Tarehe 06.01.2008
 • Mwandishi Oummilkheir
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo http://p.dw.com/p/Cl1W
 • Tarehe 06.01.2008
 • Mwandishi Oummilkheir
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo http://p.dw.com/p/Cl1W

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com