JERUSALEM:Wafungwa kadhaa wa Kipalestina waachiwa huru | Habari za Ulimwengu | DW | 01.10.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

JERUSALEM:Wafungwa kadhaa wa Kipalestina waachiwa huru

Israel imewaachia huru wafungwa kadhaa wa Kipalestina kama zawadi ya mwezi mtukufu wa Ramadhan kwa kiongozi wa mamlaka ya Palestina Mahmoud Abbas.

Magari mawili ya kijeshi yasiyokuwa na madirisha yaliwabeba wafungwa 57 wa Kipalestina kutoka jela ya Ketziot iliyo kusini mwa Israel kuelekea eneo la mpakani ya Beitunya katika eneo la Ukingo wa magharibi.

Hakuna taarifa kuwahusu wafungwa 29 wa Kipalestina wanaotoka katika eneo la Ukanda wa Gaza iwapo wataachiliwa kama ilivyopangwa hapo awali.

Baraza la mawaziri wa Israel wiki iliyopia lilipitisha kuachiliwa huru wafungwa hao wa Kipalestina kama waziri mkuu wa Israel Ehud Olmert alivyo muahidi rais wa mamlaka ya Palestina Mahmoud Abbas kabla ya mkutano wao wa mwezi November unaodhaminiwa na Marekani.

Israel inawazuilia takriba wafungwa elfu kumi na moja wa Kipalestina.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com