JERUSALEM.Bunge lajadili iwapo rais ashtakiwe
15 Februari 2007Matangazo
Wabunge wa Israel wameanza kujadili hoja inayohusu iwapo rais Moshe Katsav ashtakiwe kufuatia tuhuma za ubakaji dhidi yake.
Mkuu wa sheria wa Israel alimfahamisha rais Katsav mwezi uliopita kuwa kuna uwezekano kwa kiongozi huyo afunguliwe mashataka ya ubakaji, mapenzi ya kinguvu na kutumia vibaya madaraka.
Rais Moshe Katsav mwenye umri wa miaka 61 anahitajika kufika mbele ya taratibu za kisheria kabla ya mkuu wa sheria wa Israel kutoa uamuzi wa mwisho.
Katsav amekanusha kufanya kosa lolote na amepuuza miito inayomtaka ajiuzulu.