JERUSALEM:Benjamin Netanyahu wa chama cha Likud ateuliwa tena | Habari za Ulimwengu | DW | 15.08.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

JERUSALEM:Benjamin Netanyahu wa chama cha Likud ateuliwa tena

Kiongozi wa Upinzani wa Israel Benjamin Netanyahu ameteuliwa tena kuwa kiongozi wa chama cha mrengo wa kulia cha Likud.Kwa mujibu wa matoke ya uchaguzi wa chama wa jana waziri mkuu huyo wa zamani alipata asilimia 75 ya kura zote.Nafasi hiyo iliwaniwa na mpinzani wake mkuu Moshe Feiglin.Umaarufu wa Bwana Netanyahu umeongezeka tangu vita vya mwaka jana dhidi ya wanamgambo wa Hezbollah wa Lebanon kumalizika aidha kuimarika kwa kundi la Hamas nchini Palestina.Chama tawala cha Kadima kinazongwa na kashfa nyingi tangu kuingia uongozini.Uchaguzi wa Israel umepangwa kufanyika mwaka 2010 ila umaarufu wa Waziri Mkuu Ehud Olmert unafifia jambo linalopelekea wadadishi kuona kuwa uchaguzi huenda ukafanyika mwaka ujao.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com