1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

JERUSALEM : Wito kuwashambulia viongozi wanamgambo

18 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCrZ

Waziri wa msimamo mkali wa sera za mrengo wa kulia nchini Israel leo ametowa wito kwa waziri mkuu wa Palestina Ismail Haniyeh na viongozi wengine wanamgambo wapelekwe peponi.

Waziri huyo mpya wa Masuala ya Mikakati alieteuliwa hivi karibuni Avigdor Lieberman ameiambia radio ya taifa nchini Israel kwamba haipaswi kushambulia kambi za wakimbizi ambapo watu wanaishi kwa dhiki lakini ni afadhali kuwashambulia viongozi wa kundi la Hamas na Jihad.Amesema hao wote wanapaswa kutowekwa kwa kupelekwa peponi pamoja.

Kiongozi huyo wa msimamo mkali wa kizalendo amesema waziri wa mambo ya nje wa Palestina Mahmud Zahar sawa na Haniyeh ambaye ni mwanachama wa kundi la wanamgambo la Hamas linaloongoza serikali ya Palestina hivi sasa pia anapaswa kushambuliwa na vikosi vya Israel.