1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

JERUSALEM : Rais wa Israel yumkini kushtakiwa

Mwanasheria Mkuu wa serikali nchini Israel amependekeza kushtakiwa kwa Rasi Moshe Katsav kwa madai ya ubakaji na kutumia vibaya madaraka yake.

Uamuzi wa mwisho wa kumshataki kiongozi huyo utaweza tu kutolewa baada ya kikao ambapo Katsav atawasilisha maelezo yake.Katsav amekanusha madai hayo yaliotokana na malalamiko ya wanawake wanne ambao walifanya kazi naye wakati akiwa Rais na wakati alipokuwa waziri katika serikali ya Israel.

Rais huyo ana kinga ya kutoshtakiwa wakati akiwa madarakani na anaweza tu kushtakiwa baada ya kujiuzulu au baada ya kumalizika kwa muda wake baadae mwaka huu.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com