1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

JERUSALEM: Peretz aondoshwa kama kiongozi wa Labour

29 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CBx1

Waziri mkuu wa zamani wa Israel,Ehud Barak ameshinda duru ya kwanza ya uchaguzi wa kiongozi mpya wa chama cha Labour.Mwezi ujao katika duru ya pili ya uchaguzi atapambana na aliekuwa mkuu wa usalama,Ami Ayalon.Kiongozi wa hivi sasa wa Labour,Amir Peretz alie waziri wa ulinzi wa Israel,ameshika nafasi ya tatu katika uchaguzi uliofanywa siku ya Jumatatu.Baada ya takriban kura zote kuchaguliwa,matokeo yameonyesha kuwa Barak amejinyakulia asilimia 36 ya kura kulinganishwa na mwanasiasa mpya Ami Ayalon alieweza kupata asilimia 31.Lakini wote wawili wameshindwa kujikingia wingi wa asilimia 40 unaohitajiwa ili kuwa mshindi wa moja kwa moja. Duru ya pili ya uchaguzi itakuwa tarehe 12 mwezi Juni.Chama cha Labour ni mshirika katika serikali ya mseto ya waziri mkuu Ehud Olmert.