1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

JERUSALEM: Mwito kususia vyuo vikuu vya Israel

Mawaziri wa Israel hii leo walieleza wasiwasi wao kuhusu mito iliyotolewa nchini Uingereza kuvisusa vyuo vikuu vya Israel na bidhaa zake kwa sababu ya sera za nchi hiyo kuelekea Wapalestina. Jumatano iliyopita,Muungano wa vyuo na vyuo vikuu vya Uingereza-UCU- katika mkutano wake wa mwaka, uliunga mkono pendekezo la kuwataka wahadhiri wafikirie matokeo ya kiadili ya kushirikiana na taasisi za elimu za taifa la Israel.Pendekezo hilo limetuhumiwa vikali na serikali za Uingereza na Israel.Wakati huo huo,zaidi ya madaktari 100 wa Uingereza wametoa mwito wa kulisusa Shirikisho la Utabibu la Israel.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com